Nasaha zangu kwa kila muislamu wa kiume na muislamu wa kike ni kuitilia umuhimu swalah, kunyenyekea na kuacha kucheza ndani yake ijapo uchache tu. Hayo ni kutokana na ukubwa wa jambo la swalah, kwa sababu pia ndio nguzo ya Uislamu, ndio nguzo kuu zaidi baada ya shahaadah mbili na ndio jambo la kwanza atalofanyiwa hesabu kwalo mja siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 31
  • Imechapishwa: 02/06/2022