Alama ya usiku wa Qadar nuru kubwa kutoka mbinguni?

Swali: Je, ni miongoni mwa alama za usiku wa Qadar kwmaba usiku wake kunajitokeza nuru kutoka mbinguni ambayo hawaioni isipokuwa wale waja wema peke yake. Inanasibishwa kwamba wako baadhi ya waja wema ambao wameona nuru hii na kwamba ishara hii imetangaa kati ya watu. Nawatambua baadhi ya waja wema – nawadhania hivo na wala simtakasi yeyote mbele ya Allaah – inasemwa kwamba waliona kitu hicho. Ni upi usahihi wa alama hii? Je, alama hiyo ina msingi katika Shari´ah takasifu?

Jibu: Hatujui msingi katika Shari´ah takasifu kwamba uliyotaja katika swali ni katika alama ya usiku wa Qadar.

´Abdul-´Aziyz Aalish-Shaykh

´Abdullaah bin al-Ghudayyaan

Swaalih al-Fawzaan

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah ( 21787)
  • Imechapishwa: 24/04/2022