Sherehe usiku wa tarehe 27 Ramadhaan

Swali: Ni ipi hukumu ya kusherehekea usiku wa tarehe 27 wa Ramadhaan peke yake?

Jibu: Kusherehekea usiku wa tarehe 27 wa Ramadhaan peke yake ni Bid´ah iliyozuliwa. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo, basi atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Kilichosuniwa ni kuhuisha usiku huo kwa kufanya ´ibaadah, kutoa swadaqah na mfano wake kama zilivyo nyusiku nyingine za kumi la mwisho.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

[1] Al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah (03/60) nr. (9761)
  • Imechapishwa: 24/04/2022