al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh ni katika vipote vilivyoangamia

Swali: Tunaomba utuelezee uendaji wa kinyume unaopatikana kwa al-Ikhwaan al-Muslimuun, na uendaji wa kinyume unaopatikana kwa [Jamaa´at] at-Tabliygh. Na je, ni katika vipote viliyoangamia alivyoeleza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hili linahitajia wakati. Nimeandika vitabu kuhusu makosa ya al-Ikhwaan al-Muslimuun, visomeni. Na nimeandika vitabu vilevile kuhusu makosa ya Tabliyghiyyuun, visomeni. Ikiwa kweli mnataka haki, basi haki iko wazi. Alhamdulillaah.

Bila ya shaka yoyote, ni katika vipote alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa hawana jengine isipokuwa shirki na Bid´ah. Lakini hatusemi kuwa ni miongoni mwa watu watakaodumishwa Motoni na wala hatusemi kuwa wote wataingia Motoni. Hapana. Hili tunamuachia Allaah.

Watu wenye Bid´ah zisizokuwa za kukufurisha, wanaingia chini ya matakwa ya Allaah. Akitaka Mwenyewe, basi atawasamehe, na akitaka, basi atawaadhibu kisha mwisho wao itakuwa ni Peponi. Isipokuwa yule aliyekufa katika shirki kubwa na kufuru ya I´itiqaad au unafiki wa I´itiqaad. Hili ni jambo lingine.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=35571
  • Imechapishwa: 03/09/2020