Swali: Vipote vya leo kama Tabliygh na al-Ikhwaan [al-Muslimuun] na mengineyo ni katika vipote vya Kihizbiy? Wako katika vijia au katika Njia iliyonyooka?

Jibu: Njia iliyonyooka nayo ndiyo njia iliyoko katika haki ni wale walioko kwa yale aliAliposema [Mtume]:

“Wamegawanyika mayahudi katika mapote 71, wakagawanyika manaswara katika mapote 72 na Ummah wangu utagawanyika mapote 73. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu”. Maswahaba waliuliza: “Ni lipi hilo, ewe Mtume?” Akasema: “Ni lile nililokuwemo katika yale niliomo leo mimi na Swahaba zangu.”

Ni lile lililokuwemo Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahaba wake. Mwenye kutaka kuingia katika makundi haya aangalie matendo yao yote kama yanaafikiana na vitendi alivyokuwemo Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahaba zake? Ikiwa yahaafikiani mia kwa mia basi hapana. Baadhi yao hawakatazi kufanya urafiki na mubtadi´ah na hawamkatazi mwenye kufanya bid´ah, badala yake wanasema tusaidiane kwa yanayojenga Uislamu na tusitofautiane kwa baidhi ya tofauti zilizoko katika mambo ya ´Aqiydah na ´Ibaadah. Tofauti na Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahaba zake, wakati mmoja wao alipomuona mwenzake kavaa herizi alimkemea na kumwambia lau utakufa katika hali hiyo hutofaulu daima, wakati makundi haya hawamkatazi mshirikina na kumfanya adui kwa kuwa kafanya shirki. Tunamuomba Allaah Atuongoze sote Njia iliyonyooka.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=130109&st=0
  • Imechapishwa: 03/09/2020