Swali: Unasemaje juu ya ambaye anamsifu Imaam al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) kwamba ni Murji-ah kitu ambacho hakikuwahi kusemwa na Shaykh Ibn Baaz wala Shaykh Ibn ´Uthaymiyn? Bali walikuwa wakimsema kwa kheri. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Yule mwenye kumtuhumu al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) hakika amemdhulumu. al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) ameitumikia Sunnah kwa miaka sabini. Amefanya kazi ambayo anastahiki kushukuriwa kwayo ambayo unakafiria kuikosa kwa wengine. Ukitazama historia ya wa wale wanachuoni wa kitambo na waliokuja nyuma basi hutompata yeyote ambaye ameitumikia Sunnah kama alivofanya yeye.

Kwa hiyo yule mwenye kumtuhumu al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) maneno hayo hakika amemdhulumu na atakuja kupata malipo yake. al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema kuwa imani inazidi na kushuka na kwamba matendo yanaingia ndani ya imani. Ingawa amesema kuhusu swalah kama walivosema maimamu wengine kwamba yule mwenye kuacha kuswali kwa uvivu hakufuru. Amesema maoni haya na kuyapata nguvu, lakini kuna wengine pia waliofanya hivo. Yule mwenye kusema kwamba alikuwa Murji-ah hakika amemdhulumu na al-Albaaniy atagombana naye mbele ya Mola wake. Nimesoma yaliyoandikwa na wengine wengi, lakini sikuona yale yenye kupelekea katika tuhuma hizi. Lakini si vyenginevyo anachotaka shaytwaan  ni kuwafarikisha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Pengine nduguze mashaytwaan Hizbiyyuun na wale wenye hisia pamoja nao ndio wenye kushiriki katika haya.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 272-273
  • Imechapishwa: 04/07/2020