Kufuta uso ndani na nje ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kufuta uso kwa mikono baada ya kuomba du´aa ni mamoja ndani ya swalah au nje ya swalah?

Jibu: Haifai kufanya hivo ndani ya swalah. Ndani ya swalah kuna kitendo cha kunyanyua mikono. Isipokuwa tu katika Qunuut na baadhi ya kwenginepo. Imetajwa katika kisa cha Abu Bakr as-Swiddiyq pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuja kipindi alipokuwa anaswali akamuona ananyanyua mikono na kumhimidi Allaah. Hakukutajwa jambo la kupangusa uso. Jambo la kufuta uso limepokelewa katika baadhi ya Hadiyth ambazo ni dhaifu. Lakini Haafidhw Ibn Hajar amesema:

“Hadiyth zinazozungumzia kuhusu kufuta uso zinapeana nguvu na zinakuwa na daraja ya nzuri kupitia zengine.”[1]

Kwa hiyo hakuna neno endapo mtu atafuta uso baadhi ya nyakati na wakati mwingine akaacha kufanya hivo. Vinginevyo Hadiyth ambazo ni Swahiyh hazikutaja jambo la ufutaji.

[1] Buluugh-ul-Maraam.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 04/07/2020