Hukumu ya kula kilichochinjwa na mnaswara

Swali: Je, inajuzu kula vichinjwa vya manaswara katika wakati wetu wa sasa kwa kuzingatia kwamba wamekuwa na njia nyingi wanazotumia za kuchinja kama kutumia mashine na dawa za kulevya kwenye mchakato wa kuchinja?

Jibu: Inajuzu kula vichinjwa vyao muda wa kuwa hatujui kuwa vimechinjwa kwa njia isiyokubalika Kishari´ah. Kwa sababu asili ya vichinjwa vyao ni uhalali kama vichinjwa vya waislamu. Hilo ni kutokana na maneno ya Allaah (Ta´ala):

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَهُمْ

“Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halili kwenu na chakula chenu ni halali kwao.” (05:05)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/396)
  • Imechapishwa: 04/07/2020