Akariri kumtaja Allaah wakati wa mafundo matatu?

Swali: Je, imepokelewa kusema:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

na:

الحمد لله

“Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

wakati wa kushusha chombo?

Jibu: Hapana. Sunnah kabla ya kuanza kula aseme:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

Akimaliza kula aseme:

الحمد لله

“Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Swali: Wakati wa kunywa kwa mafundo matatu anaponyanyua chombo aseme:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

na anaposhusha aseme:

الحمد لله

“Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Kisha akinyanyua tena chombo aseme:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”?

Jibu: Hayakupokelewa haya. Ataje jina la Allaah mara moja pale mwanzoni na amshukuru Allaah pindi atapomaliza. Akikariri Allaah atamjaza kheri. Hata hivyo Sunnah inatosha mara moja tu. Ataje jina la Allaah mara moja pale mwanzoni na amshukuru Allaah pale atapomaliza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23245/حكم-تكرار-التسمية-والحمد-في-الشرب
  • Imechapishwa: 06/12/2023