Uongofu wakati maiti anapotaka kukata roho

Swali: Kuna uongofu upi kwa ambaye anataka kukata roho?

Jibu: Atamkishwe “Laa ilaaha illa Allaah”. Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Walakinisheni maiti wenu “Laa ilaaha illa Allaah”.”

Mtu amtajie “Laa ilaaha illa Allaah” mbele yake. Pale atakapoisema tu basi inatosha na hivyo wanyamaze.

Swali: Aiseme kisha wanyamaze?

Jibu: Akiisema inatosha.

Swali: Afumbwe macho yake?

Jibu: Baada ya kutoka roho yake. Ikishatoka roho yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23248/ما-الهدي-المشروع-عند-المحتضر
  • Imechapishwa: 06/12/2023