04. Hadiyth “Hakika misikiti iko na watembezi ambao Malaika… “

329 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

إنّ للمساجد أوتاداً ؛ الملائكة جلساؤهم، إنْ غابوا يفتقدونهم ، إنْ مرضوا عادوهم، وإنْ كانوا في حاجة أعانوهم

“Hakika misikiti iko na watembezi ambao Malaika ndio wanaokaa nao. Wasipojitokeza, wanawakosa. Wakiugua, wanawatembelea. Wakiwa na haja, wanawasaidia.  Kisha akasema:

جليس المسجد على ثلاث خصالٍ: أَخٌ مستفاد، أو كلمة حكمة، أو رحمة منتظَرة

“Yule anayekaa msikitini anapata mambo matatu: ima ndugu anayetoa faida, neno la hekima au rehema inayosubiriwa.”[1]

Ameipokea Ahmad kupitia kwa Ibn Lahiy´ah.

[1] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/252)
  • Imechapishwa: 06/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy