Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ : ((إِنَّ اللَّهَ يَغَارُ وَغَيْرَةُ اللَّهِ أَنْ يَأْتِيَ الْمُؤْمِنُ مَا حَرَّمَ اللَّه)) متفق عليه

64 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anaona wivu. Kuona Kwake wivu (Ta´ala) ni kule muumini kuyaendelea yale aliyomharamishia.”[1]

Katika Hadiyth hii kunapatikana faida ya kumthibitishia wivu Allaah. Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya Hadiyth kama hii na nyenginezo katika Aayah na Hadiyth za sifa ni kwamba wanamthibitishia sifa hii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa njia inayolingana na Yeye. Wanasema kuwa Allaah anaona wivu lakini hata hivyo sio kama wivu wa viumbe. Allaah anafurahi lakini sio kama furaha ya viumbe. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ana sifa kamilifu ambazo zinalingana na Yeye na hazifanani na sifa za viumbe:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖوَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kuona yote.” (42:11)

[1] al-Bukhaariy na Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/498)
  • Imechapishwa: 25/06/2023