´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa kuswali ni kujifananisha na wanamme

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega wakati wa kuswali pamoja na kuzingatia kwamba hakuna wanamme maeneo hapo?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kuweka ´Abaa´ah juu ya mabega. Kwa sababu kufanya hivo ni kujifananisha na wanamme. Imethibiti kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kwamba amewalaani wanamme wenye kujifananisha na wanawake na wanawake wenye kujifananisha na wanamme.”

Lakini ni lazima kwa mwanamke kujisitiri mwili wake ndani ya swalah kwa namna isiyokuwa hii.

Kuhusu uso imependekezwa kwa mwanamke kuacha wazi uso wake kama wanamme ikiwa mbele yake hawapo wanamme wasiokuwa Mahaarim zake. Viganja vya mikono bora ni kuvifunika kutokana na kuenea kwa dalili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/408)
  • Imechapishwa: 28/09/2021