Alama nyingine ni kutokukubali haki, kuinyenyekea na kufanya kiburi juu ya yule mwenye kusema haki, khaswa ikiwa huyo mwenye kuizungumza haki hiyo yuko chini mbele ya macho ya watu. Anaendelea kuing´ang´ania batili kwa kuchelea asikose wafuasi endapo atarejea kwenye haki. Pengine akaonyesha hadharani kimaneno kuisema vibaya nafsi yake,  lakini kwa ajili tu ya kutaka kuwaonyesha watu kuwa ni mnyenyekevu na hivyo asifiwe kwa jambo hilo. Kwa mujibu wa wanafunzi wa Maswahabah na wanazuoni wengine waliokuja baada yao mwenendo huo ni aina fulani ya kujionyesha. Hudhihiri kutoka kwao upokeaji na utafutaji wa sifa mambo ambayo yanapingana na ukweli na utakasifu wa nia. Mkweli anaogopa unafiki juu ya nafsi yake na anaichelea nafsi yake mwisho mbaya na hivyo anakuwa hana muda wa kutafuta na kukubali sifa. Kwa ajili hiyo ikawa miongoni mwa alama za watu wenye elimu yenye manufaa ni kwamba wanazidharau nafsi zao, wanachukia sifa na matapo na wala hawafanyi jeuri dhidi ya yeyote.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 28/09/2021