Ibn Battwah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Asimtii mke wake juu ya kutoka kwenda katika sherehe, kuomboleza na bafu za nje. Vivyo hivyo kuhusu kumtii katika matamanio yake mengine yote.”[1]

Haya yanahitaji kuthibiti. Hata hivyo ni jambo limekatazwa akamtii katika kila jambo kukiwemo maasi. Hata hivyo hapana neno akimtii katika jambo la halali na lisilokuwa na makatazo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa mlaini na mpole. Ilikuwa pindi ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) anapotaka kitu, basi humpa nacho. Jaabir ameeleza kuhusu hijjah ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba aliingia kwenye Ihraam kwa ajili ya kufanya ´Umrah:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwanaume mrahisi. Anapotaka jambo, basi humkubalia.”[2]

Kwa hivyo Athar iliyonakiliwa na mtunzi inakusudia kumtii katika maasi. Haifai kwa mwanaume kumtii mke wake atapomwamrisha kuwafanyia utovu wa nidhamu wazazi wake, kukata mawasiliano na ndugu zake au dhambi nyingine. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.”[3]

[1] ash-Sharh wal-Ibaanah, uk. 76.

[2] Muslim (1213).

[3] al-Bukhaariy (7258) na Muslim (1840).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Iaanah ´alaa Taqriyb-ish-Sharh wal-Ibaanah (2/792)
  • Imechapishwa: 20/08/2023