al-Haakim ameeleza kuwa amemsikia Ibn Khuzaymah akisema:

“Anashuka (Ta´ala) chini kila usiku katika mbingu ya chini na kusema:

”Kuna mwenye kuomba apewe? Kuna mwenye kuomba aitikiwe? Kuna mwenye kuomba msamaha asamehewe?”[1]

Anayedai kuwa kinachoshuka ni amri Yake amepotea. Anawazungumzisha waja Wake, bila kulifanyia namna:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

Si kama walivodai Jahmiyyah, kwamba ametawala. Allaah anawazumgisha waja Wake mwanzo na mwisho na anawakariria visa, amri na makatazo Yake. Ambaye atadai kinyume na hivo basi ni mpotevu na mzushi.”

[1] al-Bukhaariy (7494) na Muslim (758).

[2] 20:05

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/381)
  • Imechapishwa: 20/08/2023