362 – Salmaan al-Faarisiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
المسلمَ يصلي وخطاياهُ مرفوعةٌ على رأسه، كلما سجد تحاتُّ عنه، فيفرغ من صلاتِه وقد تحاتَّتْ عنه خطاياه
“Muislamu anaswali na huku makosa yake yameinuliwa juu ya kichwa chake. Kila anaposujudu, basi yanamdondoka. Anamaliza swalah yake na huku makosa yake yamemdondoka.”[1]
Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” na ”al-Mu´jam as-Swaghiyr”. Katika cheni ya wapokezi yuko Ash´ath bin Ash´ath as-Sa´daaniy ambaye sijapata wasifu wake[2].
[1] Nzuri na Swahiyh.
[2] Bali anajulikana. Ibn Hibbaan na wengine wamemzingatia kuwa ni mwenye kuaminika. Ametajwa katika ”as-Swahiyhah” 3402).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/267)
- Imechapishwa: 20/08/2023
- taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)