Aadam na mkewe (´alayhimaas-Salaam) wakiambiwa kuingia Peponi

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَقُلْنَا يَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ وَكُلَا مِنْهَا رَغَدًا حَيْثُ شِئْتُمَا وَلَا تَقْرَبَا هَـٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ

“Tukasema: “Ee Aadam, kaa wewe na mkeo Peponi na kuleni humo kwa marefu na mapana popote mpendapo na wala msiukaribie mti huu mtakuwa katika madhalimu.””[1]

Pindi alipomuumba Aadam na akamfadhilisha akamtimizia neema Yake juu yake kwa kumuumbia mke ili aweze kuishi naye na kuanasika naye. Akawaamrisha kukaa Peponi na kutulizana humo ndani ya Pepo ambayo ni pana.

حَيْثُ شِئْتُمَا

“… popote mpendapo… “

Bi maana aina mbalimbali za matunda. Allaah akamwambia:

إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعْرَىٰ وَأَنَّكَ لَا تَظْمَأُ فِيهَا وَلَا تَضْحَىٰ

“Hakika wewe humo hutopata njaa na wala hutokuwa uchi na kwamba wewe hutopata kiu humo na wala hutopata joto.”[2]

وَلَا تَقْرَبَا هَذِهِ الشَّجَرَةَ

“… wala msiukaribie mti huu… “

Ni aina miongoni mwa aina ya miti ya Peponi. Allaah ndiye anajua zaidi juu yake. Aliwakataza mti huo kwa ajili ya kuwapa mtihani na majaribio au kwa sababu ya hekima tusiyoijua sisi.

فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ

“… mtakuwa katika madhalimu.”

Ni dalili inayojulisha kuwa makatazo yalikuwa kwa njia ya uharamu. Kwa sababu makatazo hayo yamepelekea katika dhuluma.

[1] 02:35

[2] 20:118-119

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 39-40
  • Imechapishwa: 16/06/2020