Ibn ´Uthaymiyn kuhusu maiti na aliyehai kupeana viungo vyao

Swali: Je, kupeana viungo ni jambo linajuzu?

Jibu: Kupeana viungo vya maiti ni haramu na haijuzu. Kwa sababu Allaah ameufanya mwili wa mtu ni amana kwake. Amesema (´Azza wa Jall):

وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ

“Wala msiziue nafsi zenu.”[1]

Katika suala la kupeana viungo hakuna tofauti kwa ambaye yuko hai na ambaye ni maiti. Nikisema hivi nina maana ya kwamba haijuzu kwa mtu aliye hai kupeana chochote katika viungo vyake kama ambavo haijuzu kwa maiti kupeana chochote katika viungo vyake. Vilevile familia yake hawana haki yoyote ya kupeana chochote katika viungo vyake baada ya kufa kwake. Familia wanachorithi ni mali. Kuhusu viungo vya maiti ni haramu. Haijalishi kitu hata kama warithi watatoa idhini ya kumkata viungo maiti ili kuvipeana haitofaa. Bali wanachuoni wa Fiqh (Rahimahumu Allaah) wamesema katika vitabu vyao katika “Kibaat-ul-Janaa-iz”:

“Haijuzu kuchukua chochote katika viungo vyake hata kama ataacha ameusia hilo.”

Hata kama maiti ameusia kuchukuliwe kiungo chake fulani haitofaa kutekeleza wasia huu. Kwa sababu mwili wa mtu ni amana. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kukata kiungo cha maiti ni kama kukikata akiwa hai.”

Kama ambavyo haijuzu kukata mfupa wa aliyehai vivyo hivyo haijuzu kukata mfupa wa maiti.

[1] 04:29

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (50) http://binothaimeen.net/content/1144
  • Imechapishwa: 16/06/2020