Twawaaf-ul-Wadaa´ baada ya ´Umrah

Swali: Mtu ambaye amefanya ´Umrah ni lazima afanye Twawaaf-ul-Wadaa´?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuwajibishia mwenye kuhiji peke yake kumaliza kwa Twawaaf-ul-Wadaa´. Haikuthibiti kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha wale wenye kufanya ´Umrah wafanye Twawaaf-ul-Wadaa´. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya ´Umrah mara nne na haikuthibiti kuwa alifanya Twawaaf-ul-Wadaa´.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2020