99. Kujifananisha kwa uinje kunapelekea kujifananisha kimaadili na kimatendo

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Nimebainisha pia kwamba kujifananisha katika mambo ya nje kunapelekea kujifananisha katika maadili na matendo. Kwa ajili hiyo ndio maana tukakatazwa kujifananisha na makafiri, wasiokuwa waarabu na maadui. Vilevile kila mmoja katika wanaume na wanawake amekatazwa kujifananisha na mwengine. Mwanaume mwenye kujifananisha na wanawake huiga maadili yao kwa mujibu wa kujifananisha kwake mpaka hatimaye ikampelekea kuwa na tabia za kikekike na kujimakinisha nafsi yake kana kwamba ni mwanamke. Wakati ilipokuwa nyimbo zinapelekea katika mambo hayo na zikawa ni miongoni mwa matendo ya wanawake, walikuwa wakiwaita wanaume wenye kuimba makhanithi.

Na mwanamke mwenye kujifananisha na wanaume huchukua tabia mpaka mpaka akaonekana kuonyesha mapambo, kujidhihirisha na kujifananisha na wanaume mpaka mwishowe ikawapelekea baadhi yao kuonyesha miili yao kama wanavyoonyesha wanaume, akapambana kuwa juu ya wanaume kama ambavo wanaume wanavokuwa juu ya wanawake na akafanya matendo na mambo yanayopingana na staha na ulinzi uliowekwa katika Shari´ah kwa wanawake. Yote haya yanaweza kupatikana kutokana na lile jambo la kujifananisha peke yake.

Tunachotaka kusema kwa haya ni kwamba ni lazima kuwepo na tofauti kati ya mavazi ya wanaume na mavazi ya wanawake inayopambanua wanaume kutokana na wanawake na kwamba mavazi ya wanawake yawe na sitara na kujifunika ipasavyo kufikia malengo. Zaidi ya hayo, haifai kwa wanawake kuvalia mavazi ambayo kwa kiasi kikubwa yamekaa kama ya kiume ingawa yatakuwa yenye kusitiri, kama mfano wa mashati marefu ambayo hutumiwa kama desturi na wanaume katika baadhi ya miji. Vilevile makatazo ya mfano wa haya yanabadilika kwa kubadilika zile desturi. Lakini yale ambayo tofauti inarejea katika sitara kama sitara, basi wanawake wataamrishwa kuvalia yale ambayo yanasitiri vyema zaidi ingawa tofauti kati ya hao wawili itaonekana vinginevyo. Kwa hivyo ikiwa vazi limekusanya uchache wa sitara na kujifananisha, basi likatazwa kutokana na mitazamo yote mawili – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.”[1]

[1] al-Kawaakib (93/132-134) ya Ibn ´Urwah al-Hanbaliy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 25/10/2023