Swali 58: Ni vita vipi vilitokea mwaka wa saba?

Jibu: Mwanzoni mwa mwaka huo vilianza vita vya Dhuu Qarad. Maoni hayo ndio yamechaguliwa na al-Bukhaariy, ambayo ndio sahihi.

Kisha baada yake kukatokea vita vya Khayar vilivyoendelea kwa miaka mitatu, kama alivoyatamka hayo wazi Salamah bin al-Akwa´. Hakuna Swahabah yeyote katika wale waliokula kiapo cha utii chini ya mti aliyevikosa, isipokuwa tu Jaabir bin ´Abdillaah. Pamoja na hivo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimuahidi thawabu na sehemu ya ngawira za vita. Ngome za jiji hilo zilitekwa na mali yake kuchukuliwa, ambapo nusu iligawiwa kwa wapambanaji na nusu nyingine ilikwenda kwa wale wenye mahitaji. Wengine ambao hawakuwepo pia waligawiwa sehemu za ngawira za vita baada ya idhini ya wale waliokuwepo. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliwaruhusu watu wa Khaybar kubaki katika mji kwa kuwapa waislamu malipo ya nusu ya mavuno ya mji huo. Wakati wa vita hivyohivyo ndio kuliharamishwa nyama ya punda vihongwe na ndoa ya Mut´ah. Kuna maoni mengine yanayosema kwamba ndoa ya Mut´ah iliharamishwa baada ya hapo. Kipindi hicho ndio kulitokea tukio la kondoo aliyetiwa sumu na maneno yake. Vilevile Ja’far bin Abiy Twaalib na Wahajiri hao walirudi kutoka Uhabeshi pamoja na wajumbe kutoka katika kabila la Ash’ar. Baada ya kurudi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akaishi kijumba na Swafiyyah.

Mwaka huohuo ndipo Abu Hurayrah akaingia katika Uislamu.

Akazingira (Swalla Allaahu ´alayhi sallam) bonde la Quraa na akataamiliana nao kama alivofanya kwa wakazi wa Khaybar. Aidha Allaah (Ta´ala) akamtunuku Fadak ambayo ilikamatwa pasi na farasi wala wapanda farasi kwenda mbio.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 120-122
  • Imechapishwa: 24/10/2023