Hadiyth za kusamehewa madhambi yaliyoko mbele

Baadhi ya wanachuoni wamesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo alipewa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake ni kuwa Allaah amemsamehe madhambi yake yaliyotangulia na yanayokuja mbele. Kujengea juu ya hili, Hadiyth yoyote inayokuja na kusema mwenye kufanya kadhaa anasamehewa madhambi yaliyotangulia na yanayokuja mbele ni dhaifu. Kwa sababu haya ni mambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhusiana na Hadiyth zenye kusema:

“Atasamehewa madhambi yaliyotangulia”

ziko nyingi. Lakini:

“… na madhambi yaliyoko mbele.”

ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Hii ni kanuni ya kijumla na yenye faida kwa mwanafunzi. Anatakiwa kutambua kuwa akijiwa na Hadiyth juu ya kwamba mwenye kufanya kadhaa atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia na yaliyoko mbele, neno:

“… na yaliyoko mbele.”

ni dhaifu na si Swahiyh. Kwa sababu hili ni katika mambo maalum aliyopewa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/73)
  • Imechapishwa: 24/10/2023