100. Haifai jilbaab kufanana na vazi la wanawake wa kikafiri

Sharti ya saba ya jilbaab ni kwamba isifanane na mavazi ya wanawake wa kikafiri. Ni jambo limethibiti katika Shari´ah, kwamba haijuzu kwa waislamu, wa kiume na wa kike, kujifananisha na makafiri. Ni mamoja kujifananisha huko ni katika ´ibaadah zao, sikukuu zao au nguo ambazo ni maalum kwao. Kwa masikitiko makubwa waislamu wengi hii leo wameacha kanuni hii tukufu, kukiwemo wale wanaopatiliza mambo ya dini na ulinganizi, kwa sababu ya ujinga juu ya dini yao au kwa sababu ya kufuata matamanio yao au kutumbukia ndani ya desturi za sasa na kufuata kichwa mchunga ada za makafiri wa ulaya. Kujifananisha huku ikawa ni moja miongoni mwa sababu za kudhalilika kwa waislamu na kuwa wanyonge na wengine kuwa na utawala na ukoloni juu yao:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ

“Hakika Allaah hayabadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe kwanza wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao.”[1]

Kanuni hii muhimu inasapotiwa na dalili nyingi ndani ya Qur-aan na Sunnah. Licha ya kwamba dalili za Qur-aan zimekuja kwa njia ya kuenea, zinafasiriwa na kubainishwa na dalili za Sunnah.

[1] 13:11

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnaja.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 161
  • Imechapishwa: 25/10/2023