101. Wanafurahi pindi waislamu wanawaigiliza

Miongoni mwa dalili za Qur-aan ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ وَآتَيْنَاهُم بَيِّنَاتٍ مِّنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

”Hakika Tuliwapa wana wa israaiyl Kitabu na Hekima na unabii na tukawaruzuku katika vizuri na tukawafadhilisha juu ya walimwengu na tukawapa hoja zinazobainisha mambo. Basi hawakutofautiana isipokuwa baada ya kuwajilia elimu kwa kufanyiana uadui na husuda kati yao. Hakika Mola wako atahukumu kati yao siku ya Qiyaamah katika yale waliyokuwa wakitofautiana.  Kisha tukakuwekea Shari´ah ya mambo, hivyo basi ifuate na wala usifuate matamanio ya wale wasiojua.”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Allaah (Subhaanah) ameeleza kuwa aliwaneemesha wana wa israaiyl neema za dini na za dunia na kwamba walitofautiana baada ya wao kuwajilia elimu kwa kufanyiana uadui wao kwa wao. Kisha Akamwekea Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) njia ya Shari´ah ya amri na akamwamrisha kuifuata na akamkataza kufuata matamanio ya wale wasiojua. Ameingia katika wale wasiojua kila ambaye amekwenda kinyume na Shari´ah Yake. Matamanio yao yanaingia yale yote wanayoyatamani na yale waliyomo washirikina kutokana na uongofu wao wa dhahiri ambao unapelekea katika dini yao ya batili. Kuafikiana nao katika mambo hayo kunamaanishwa kufuata yale matamanio yao. Kwa ajili hiyo makafiri hufurahi pale ambapo wanawaona waislamu wanaafikiana nao katika baadhi ya mambo yao. Wangelipenda kutumia pesa nyingi ili waislamu waweze kuwaigiliza. Lau itadhaniwa kuwa kitendo fulani sio katika kufata matamanio yao, hapana shaka yoyote kwamba kwenda nao kinyume ndio bora kwa ajili ya kufunga zile njia zote za kufuata matamanio yao na pia kwa ajili ya kufikia radhi za Allaah kwa kuyaacha. Jengine ni kwa sababu kuwaigiliza katika mambo hayo kunaweza kupelekea kuwaigiliza katika mambo mengine.”[2]

Pasi na kuangalia lengo linafikiwa kwa jumla ingawa chaguo la kwanza ndio liko wazi zaidi.”

[1] 45:16-18

[2] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 8

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 25/10/2023