Kupinga Hadiyth kwa kutumia akili – mtindo wa Ahl-ul-Bid´ah

Swali: Vipi kwa ambaye anarudisha nyuma sehemu kubwa ya Hadiyth kwa kutumia akili?

Jibu: Hakuna wenye kuona hivo isipokuwa wanafalsafa. Hiyo ni dhambi. Bali ni lazima kuifanyia kazi kwa mujibu wa njia zake zinazokubalika katika Shari´ah; kwa njia ya maimamu wa Hadiyth na kutafiti cheni za wapokezi wake. Ni batili kuifanya akili ndio yenye kuamua. Ni miongoni mwa matendo ya Jahmiyyah na mfano wao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23068/حكم-رد-الاحاديث-النبوية-بالعقل
  • Imechapishwa: 25/10/2023