Kudumisha swalah ya Dhuhaa

Swali: Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Kila kiungo cha mwili wa mmoja wenu kinapambaukiwa kutoa swadaqah. Kila Tasbiyh ni swadaqah, kila Tahmiyd ni swadaqah, kila Tahliyl ni swadaqah, kila Takbiyr ni swadaqah, kuamrisha mema ni swadaqah na kukataza maovu ni swadaqah. Zinamtosheleza kutokana na hayo Rak´ah mbili anazorukuu za Dhuhaa.”[1]

Rak´ah mbili hizi ndio uchache wa Rak´ah za Dhuhaa?

Jibu: Sahihi, ndio uchache wake. Ni sawa pia akiswali Rak´ah nne, sita, nane au kumi. Wakati wote wa mchana kabla ya adhuhuri ni wakati wa kufanya ´ibaadah. ´Amr bin ´Absah amesimulia kuwa amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ukiswali Subh basi jizuilie kuswali mpaka kuchomoza kwa jua. Kisha swali, kwani hakika swalah ni yenye kushuhudiwa na yenye kuhudhuriwa mpaka jua linaposimama jua.”

Swali: Imesuniwa kudumu kuiswali?

Jibu: Ndio, imesuniwa kuidumisha.

[1] Muslim (720).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23069/ما-اقل-عدد-ركعات-صلاة-الضحى
  • Imechapishwa: 25/10/2023