99. Athar ”Ibn ´Umar alikuwa alipofika kutoka safarini… ”

100 – Sulaymaan bin Harb ametuhadithia: Hammaad bin Zayd ametuhadithia, kutoka kwa Ayyuub, kutoka kwa Naafiy´, ambaye amesema:

”Ibn ´Umar alikuwa alipofika kutoka safarini, basi huingia msikitini. Kisha akaliendea kaburi na kusema:

السلام عليك يا رسول الله، السلام على أبي بكر، السلام على أبي

”Amani iwe juu yako, ee Mtume wa Allaah! Amani iwe juu yako, ee Abu Bakr! Amani iwe juu yako, ee baba yangu kipenzi!”

Halafu akaswali Rak´ah mbili.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. al-Bayhaqiy ameipokea kupitia kwa Yuusuf bin Ya´quub al-Qaadhwiy: Sulaymaan bin Harb ametuhadithia…

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 84
  • Imechapishwa: 19/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy