100. Athar ”Hakuna alfajiri inayopambazuka… ”

102 – Mu´aadh bin Asad ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia: Ibn Lahiy´ah ametukhabarisha: Khaalid bin Yaziyd amenihadithia: kutoka kwa Sa´iyd bin Abiy Hilaal, kutoka kwa Munabbih bin Wahb, ambaye amesimulia:

”Ka´b aliingia kwa ´Aaishah, wakamtaja Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ka´b akasema: ”Hakuna alfajiri inayopambazuka isipokuwa wanashuka Malaika 70.000, ambapo wanalizunguka kaburi, wanapiga kwa mbawa zao na wanamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Inapofika jioni, wanapanda na wakashuka Malaika wengine 70.000, wakalizunguka kaburi, wakapiga kwa mbawa zao na wakamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). 70.000 usiku na 70.000 mchana. Wakati ardhi inapasuka wakaiharakia Malaika 70.000.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni yenye kukatika. Wapokezi wake wote ni wapokezi wa al-Bukhaariy na Muslim. Hata kama al-Bukhaariy na Muslim wamemtumia Sa´iyd bin Abiy Hilaal kama hoja, Ahmad amesema juu yake:

”Sijui ana nini. Anazichanganya Hadiyth.”

Ibn Lahiy´ah ni dhaifu isipokuwa katika yale ambayo wale ´Abdullaah watatu wamepokea kutoka kwake, na hii ni katika hizo kwa vile ´Abdullaah bin al-Mubaarak amesimulia kutoka kwake. Abu ´Abdir-Rahiym Khaliyd bin Yaziyd al-Jamhiy al-Miswriy ni mwaminifu na ni katika wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim. Wale ´Abdullaah watatu ni ´Abdullaah bin al-Mubaarak, ´Abdullaah bin Wahb na ´Abdullaah bin Yaziyd al-Muqriy’.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 19/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy