101. Athar ”Sitajwi mimi isipokuwa nawe utatajwa… ”

103 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: Ibn Abiy Najiyh ametuhadithia, kutoka kwa Mujaahid, ambaye amesema kuhusu:

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ

“Tukanyanyulia juu utajo wako.”?[1]

”Sitajwi mimi isipokuwa nawe utatajwa. Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.”[2]

[1] 94:04

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. Wanamme wote ni wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim. Ibn Abiy Najiyh jina lake ni ´Abdullaah. Sufyaan ni Ibn ´Uyaynah. ´Aliy bin ´Abdillaah ni Ibn-ul-Madiyniy. Katika Hadiyth Allaah (Jalla wa ´Alaa) ndiye anayemzungumzisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo Hadiyth imesimuliwa kutoka kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 86
  • Imechapishwa: 19/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy