Haya ndio makusudio yake Mtume kuogopa mtihani wa wanawake

Swali: Ni yepi makusudio kwamba wana wa israaiyl mtihani wao ulikuwa kwa sababu ya wanawake? Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hivyo basi, iogopeni dunia na waogopeni wanawake.”[1]

Jibu: Malengo ni kwamba tuwachukulie hatua wanawake; tusiwaache wakafanya watakavyo:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ

“Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake.”[2]

Amsimamie mwanamke, amuhifadhi kutoonyesha mapambo, kutoka nje na kusafiri bila Mahram. Kwa sababu yeye ndiye mwenye kumsimamia na anamuhifadhi. Asimpuuze na akampa uhuru, kama wanavosema. Huo ni utumwa, na sio uhuru. Uhuru ni kwa Uislamu, kumwabudu Allaah Mmoja pekee na kujiepusha na mambo ya haramu. Huo ndio uhuru.

[1] Muslim (2742)

[2] 04:34

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 19/02/2024