Swali: Baadhi ya ndugu katika baadhi ya miji ya Kiislamu wanavunja makaburi na mapango kwa lengo la kuamrisha mema na kukemea maovu.

Jibu: Hili ni kosa. Ni kosa kubwa. Makaburi hayavunjwi isipokuwa na mtawala. Hayavunjwi na watu wa kawaida. Kwa sababu kitendo hicho kinazua shari na likajengwa kaburi imara zaidi kuliko walilokuwa nalo hapo kabla. Matokeo yake haileti faida yoyote. Pengine kikazuia fitina, magomvi na shari kwa Ahl-us-Sunnah. Kwa hivyo makaburi hayavunjwi isipokuwa na watawala. Zingatieni hilo.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa Makkah kabla ya kuhajiri. Ka´bah na baina ya Swafaa´ na Mawra kwenyewe yalikuweko masanamu 360. Hakuyashambulia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akitufu Ka´bah, akiswali na akimuomba Allaah na wala hakuyashambulia masanamu ilihali yeye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu hakuna na madaraka. Wakati alipohama kwenda Madiynah na Allaah akamjaalia kuuteka mji wa Makkah, kitu cha kwanza alichoanza nacho ni kuyabomoa na kuyavunja masanamu. Baada ya kuwa na madaraka na nguvu… kwa sababu yeye ndiye mtawala sasa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na hakuna yeyote aweza kupingana naye. Hapo ndipo aliyavunja. Ikafahamisha kuwa kuyavunja masanamu, mizimu, makaburi na mapango ni kazi ya mtawala wa Kiislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 19/02/2024