104 – Muhammad bin ´Ubayd ametuhadithia: Muhammad bin Thawr ametuhadithia, kutoka kwa Ma´mar, kutoka kwa Qataadah, ambaye amesema kuhusu:

وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ

“Tukanyanyulia juu utajo wako.”[1]?

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Anza na utumwa kisha fuatisha ujumbe.”

Ma´mar amesema: ”Nashuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni mja Wake. huu ndio utumwa. Ujumbe ni kule mtu kusema kuwa yeye ni mja na Mtume Wake.”[2]

[1] 94:04

[2] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh lakini kuna Swahabah anayekosekana. Wanamme wake wote ni waaminifu.

  • Muhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 20/02/2024
  • Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy