97. Athar ”Nilimuona ´Abdullaah bin ´Umar akisimama karibu na kaburi la Mtume… ”

98 – ´Abdullaah bin Maslamah ametuhadithia, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa ´Abdullaah bin Diynaar, ambaye amesema:

”Nilimuona ´Abdullaah bin ´Umar akisimama karibu na kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akimuombea du´aa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Tamko hili amelipokea Maalik. Kupiti kwake al-Bayhaqiy amepokea kwa tamko lisemalo:

”Asimame karibu na kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha amsalimie Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), amuombee du´aa Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa).”

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 83
  • Imechapishwa: 15/02/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy