84. Ndio maana ikakatazwa mwanamke kutoka amejipaka manukato

Sababu ya makatazo iko wazi kwa sababu harufu nzuri na manukato yanaamsha matamanio. Wanazuoni wameimbatanisha dhambi hiyo na madhambi kama ya mavazi ya marembo, vito vinavyoonekana na kuchanganyika na wanamme[1]. Ibn Daqiyq-il-´Iyd amesema:

”Kunafahamisha kuwa ni haramu kwa wanawake wanaotaka kwenda kuswali msikitini kujitia manukato, kwa sababu kunahamasisha matamanio ya wanamme.”[2]

Ikiwa ni haramu kwa mwanamke anayetaka kwenda kuswali msikitini kujitia manukato, hukumu inakuweje kwa anayetaka kwenda sokoni na mitaani? Hapana shaka kuwa uharamu wake ni mkubwa na dhambi yake ni kubwa zaidi. al-Haythamiy amethibitisha kuwa ni dhambi kubwa kwa mwanamke kutoka hali ya kuwa amejitia manukato na amejipamba, haijalishi kitu hata kama mume wake atampa ruhusa[3].

Isitoshe Hadiyth hizi ni zenye kuenea na zinahusu nyakati na maeneo yote. Hadiyth ya tatu imetaja ´Ishaa kwa sababu tu fitina yake kipindi hicho inakuwa kubwa zaidi. Kwa maana nyingine ni kwamba mtu asikifirie kuwa kitendo hicho kinafaa akitoka katika nyakati zingine. Ibn-ul-Maalik amesema:

”Kinachodhihiri ni kwamba makatazo yametajwa wakati huo kwa sababu ni wakati wa giza na njia zinakuwa tupu. Manukato yanaamsha matamanio. Kwa ajili hiyo mwanamke hawezi kuhisi salama kwa aina mbalimbali ya mitihani, tofauti na wakati wa asubuhi na jioni. Isitoshe tumeshatangulia kusema kuwa ni haramu kabisa kwa mwanamke kuhudhuria msikitini ikiwa amejitia manukato.”[4]

[1] Tazama ”Fath-ul-Baariy” (2/279).

[2] Tazama ”Faydhw-ul-Qadiyr” ya al-Munaawiy na maelezo yake ya ile Hadiyth ya kwanza ya Abu Hurayrah.

[3] Tazama ”az-Zawaajir” (2/37).

[4] Tzama ”al-Mirqaat” (2/71) ya Shaykh ´Aliy al-Qaariy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 139-140
  • Imechapishwa: 17/10/2023