Sharti ya tano ya jilbaab ni kwamba isiwe yenye kutiwa harufu nzuri na manukato. Zipo Hadiyth nyingi zinazomuharamishia mwanamke kujitia manukato pindi anapotoka nyumbani. Hapa tutakuorodheshea zile ambazo imesihi cheni ya wapokezi wake:

”Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke yeyote atakayejipaka manukato na akawapitia watu ili wapate kuhisi harufu yake, huyo ni mzinifu.”

2 – Zaynab ath-Thaqafiy amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Anapotoka mmoja wenu kwenda msikitini, basi asikaribie manukato.”[1]

3 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanamke yeyote atakayejifukiza uvumba, basi asiswali pamoja nasi ´Ishaa.”[2]

4 – Muusa bin Yasaar amesimulia:

”Mwanamke mmoja aliyejipaka mafuta alipita karibu na Abu Hurayrah ambaye akasema: ”Ee kijakazi wa al-Jabbaar! Unaelekea msikitini?” Akajibu: ”Ndio.” Akasema: ”Ndio maana umejitia manukato?” Akajibu: ”Ndio.” Akasema: ”Basi rejea na uoge. Kwani hakika mimi nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Hakuna mwanamke yeyote anayetoka kwenda msikitini, isipokuwa Allaah huirudisha swalah yake mpaka atakaporejea nyumbani na kuoga.”[3]

[1] Muslim, Abu ´Awaanah, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo. Nimezungumzia cheni ya wapokezi wake katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab” na ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah”.

[2] Muslim, Abu ´Awaanah, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, at-Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo.

[3] al-Bayhaqiy (3/133) na (3/246) kupitia kwa al-Awzaa´iy kutoka kwa Muusa bin Yasaar.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 137-138
  • Imechapishwa: 17/10/2023