Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ngazi ya kwanza: Uislamu una nguzo tano: Kushuhudia ya kwamba hapana mungu anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba ya Allaah tukufu.

MAELEZO

Uislamu hauwezi kusimama isipokuwa juu ya nguzo hizi. Zikikosekana basi Uislamu hauwezi kusimama. Matendo mengine ni yenye kukamilisha nguzo hizi. Matendo mema mengine yote ni yenye kukamilisha nguzo hizi. Kwa ajili hii Jibriyl alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mbele ya Maswahabah kwa kusema:

“Nieleze juu ya Uislamu.” Akamjibu: “Uislamu ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa kweli isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga Ramadhaan na kuhiji Nyumba kwa yule mwenye uwezo wa kuiendea.”

Kwa hiyo akafasiri Uislamu kwamba ni hizi nguzo tano. Lakini Hadiyth ya Ibn ´Umar imebainisha kuwa mambo haya matano ndio yenye kujenga Uislamu pale aliposema:

“Uislamu umejengwa juu ya mambo matano… “[1]

Bi maana Uislamu mzima si mambo haya matano. Lakini mambo hayo ndio nguzo ambazo Uislamu umejengeka juu yake na mambo mengine yaliyowekwa katika Shari´ah ni yenye kukamilisha nguzo hizi.

[1] al-Bukhaariy (08) na Muslim (16).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 162-163
  • Imechapishwa: 06/01/2021