Swali: Mwenye kuhudhuria kwenye maulidi anapata dhambi ijapo lengo lake ni kwa ajili ya kula?

Jibu: Haijuzu kuhudhuria. Ukihudhuria umewapata nguvu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, afanye hivo kwa moyo  wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

Kukemea kwa moyo haina maana kwamba ukaketi chini. Sivyo hivyo. Unatakiwa kubadilisha sehemu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (104) https://www.alfawzan. af.org.sa/sites/default/files/13-03-1441%D9%87%D9%80~1_0.mp3
  • Imechapishwa: 05/01/2021