80. Kila daraja ina nguzo zake na maana ya nguzo

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kila daraja ina nguzo zake.

MAELEZO

Kila daraja… – Nguzo ni kitu ambacho kingine husimama juu yake. Nguzo za kitu ni zile pande zake ambazo husimama juu yake na wala hazisimami zikikosekana na zinakuwa ndani ya kitu tofauti na masharti ambayo yanakuwa nje ya kitu. Kwa mfano masharti ya swalah ambayo yanakuwa nje na kabla ya swalah. Kuhusu nguzo za swalah zinakuwa ndani yake. Ni kama mfano wa Takbiyrat-ul-Ihraam na usomaji wa al-Faatihah. Kukiharibika kitu katika hayo basi swalah haisihi. Ni kama ambavo kukiharibika kitu katika nguzo za nyumba basi haiwezi kusimama na wala haisimami.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 05/01/2021