Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ihsaan

MAELEZO

Hii ndio ngazi ya tatu ambayo ni Ihsaan. Ni kule mja kufanya vizuri kwa yale yaliyoko baina yake yeye na Allaah wakati wa kumwabudu Allaah (´Azza wa Jall). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametaja Ihsaan kwa kusema:

“Ihsaan ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona na ikiwa wewe humuoni basi tambua kuwa Yeye anakuona.”[1]

Bi maana unatakiwa uwe na elimu ya yakini kwamba Allaah anakuona popote unapokuwa.

[1] al-Bukhaariy (50) na Muslim (09 na 10).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 161
  • Imechapishwa: 05/01/2021