Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

imani

MAELEZO

Hii ndio ngazi ya pili. Waumini wanatofautiana. Miongoni mwao wako wale wenye kujikurubisha na miongoni mwao wako wale wema. Wenye kujikurubisha ndio watu wenye daraja za juu zaidi. Wema wako chini yao. Miongoni mwao wako wale wenye kujidhulumu nafsi zao. Hawa ni wale wenye kufanya madhambi makubwa ambayo ni chini ya shirki. Hawa ni waumini watenda madhambi. Pia wanaweza kuitwa waumini wenye imani dhaifu. Amesema (Ta´ala):

ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا ۖ فَمِنْهُمْ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِ وَمِنْهُم مُّقْتَصِدٌ وَمِنْهُمْ سَابِقٌ بِالْخَيْرَاتِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَضْلُ الْكَبِيرُ

“Kisha Tukawarithisha Kitabu wale tuliowateuwa miongoni mwa waja Wetu. Basi miongoni mwao ni aliyedhulumu nafsi yake na miongoni mwao aliyekuwa kati na kati na miongoni mwao aliyetangulia kwa mambo ya kheri kwa idhini ya Allaah – hiyo ndio fadhilah kubwa.”[1]

[1] 35:32

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 160
  • Imechapishwa: 05/01/2021