77. Mkono wa kuume wa Allaah umejaa

76 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kwa kutoa mchana na usiku. Mnaonaje yale Aliyotoa tangu aumbe mbingu na ardhi pasi na kupungua chochote kilichoko katika mkono Wake wa kuume? ´Arshi Yake iko juu ya maji na kwenye mkono Wake mwingine kuna mzani ambao ndiyo anashusha na kupandisha.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 115
  • Imechapishwa: 30/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy