Kulia na kuhuzunika bila ya kunyanyua sauti na kutoa maneno ya haramu hakupingani na kusubiri na kuridhia, kama tulivyotoka kutaja punde tu. Allaah (Ta´ala) ameeleza kuhusu Ya´quub (´alayhis-Salaam):

وَابْيَضَّتْ عَيْنَاهُ مِنَ الْحُزْنِ فَهُوَ كَظِيمٌ

“Macho yake yakageuka meupe [kwa kulia] kutokana na huzuni.” (12:84)

Qataadah amesema:

“Huzuni wake daima ulikuwa ndani pasi na kutoa neno hata moja. Hakusema lolote isipokuwa kheri.”

Allaah (Ta´ala) amesema kuwa alisema:

إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Hakika mimi machozi na huzuni wangu namshitakia Allaah na najua kutoka kwa Allaah kitu msichokijua.” 12:86

فَصَبْرٌ جَمِيلٌ

“Subira ni njema… “ 12:83

Imepokelewa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kushtakia huzuni wake hakusubiri.”

Pamoja na kuwa Ya´quub (´alayhis-Salaam) alipoteza macho yake kwa sababu ya kulia, huzuni na kulia kwake hakukupingana na subira yake. Hakika (´alayhis-Salaam) alimshtakia Allaah huzuni wake na si kiumbe. Ibn ´Abbaas ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huzuni wake daima ulikuwa ndani pasi na kutoa neno hata moja. Hakusema lolote isipokuwa kheri.”

Allaah (Ta´ala) amesema ya kwamba alisema:

إِنَّمَا أَشْكُو بَثِّي وَحُزْنِي إِلَى اللَّـهِ وَأَعْلَمُ مِنَ اللَّـهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

“Hakika mimi machozi na huzuni wangu namshitakia Allaah na najua kutoka kwa Allaah kitu msichokijua.” 12:86

فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا

“Subiri subira njema!” 70:05

Imepokelewa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kushtakia huzuni wake hakusubiri.”

Pamoja na kuwa Ya´quub (´alayhis-Salaam) alipoteza macho yake kwa sababu ya kulia, huzuni na kulia kwake hakukupingana na subira yake. Hakika (´alayhis-Salaam) alimshtakia huzuni wake na Allaah si kiumbe. Ibn ´Abbaas amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ama kile kinachotoka kwenye macho na moyo kinatoka kwa Allaah ( Azza wa Jall) na huruma. Na kile chenye kutoka kwenye mkono na ulimi ni kutoka kwa shaytwaan.”

Khaalid bin Abiy ´Uthmaan al-Qurashiy amesema:

“Sa´iyd bin Jubayr alinipa pole pindi mtoto wangu alipofariki. Katika mnasaba fulani akaniona natufu Ka´bah hali ya kuwa niko na maski. Akanivua nayo kichwani na kusema: “Kujificha ni kukata tamaa.”

Bakr al-Muzaniy amesema:

“Ilikuwa inasemwa kukaa nyumbani baada ya msiba ni katika kukata tamaa.”

´Ubayd bin ´Umar amesema:

“Kukata tamaa sio kutokwa na machozi na kuwa na huzuni moyoni. Kukata tamaa ni kutoa maneno machafu na dhana mbaya.”

Kuna mtoto wa Qaadhiy aliyefariki Baswrah na wanachuoni wa mji wakakusanyika na wakazungumzia nini kukata tamaa kunakopingana na subira. Wakaafikiana kwamba mtu akiacha kitu baada ya msiba katika yale mambo aliyozowea kufanya amekata tamaa.

Ibn ´Abdil-´Aziyz amesema:

“Alifariki mtoto wangu mwenye thamani. Akamwambia mama yake: “Mche Allaah, tarajia malipo kutoka kwa Allaah na vuta subira.” Akamwambia: “Msiba wangu kwake ni mkubwa kwa mimi kuuharibu na kukata tamaa.”

Ibn-ul-Mubaarak amesema:

“Kuna mwanaume alikuja kwa Yaziyd bin Yaziyd ambaye alikuwa anaswali na huku mtoto wake yuko anataka kufa. Mwanaume yule akamwambia: “Unaswali ilihali mtoto wako yuko anataka kufa?” Akamwambia: “Mtu akiwa na mazowea ya kufanya kitu na akakiacha siku moja tu, inazingatiwa kuwa ni kasoro katika kitendo chake.”

Thaabit amesema:

“´Abdullaah bin Mutwarrif alifikwa na msiba na nikaona alama nzuri na bora kabisa kwake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 165-166
  • Marejeo: Firqatunnajia.com
  • Imechapishwa: 12/11/2016