Swali: Mwanafunzi akihudhuria kwenye darsa hili lakini pasi na ridhaa ya wazazi wake ambao wamemuomba awafikishe sehemu fulani ambapo akawa amekataa na badala yake akahudhuria kwenye darsa hili. Ni ipi hukumu? Una mnasihi vipi?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya hivo. Alitakiwa ampeleke baba yake hata kama atachelewa darsa. Kumtendea mzazi wema ndio kunatakiwa kupewa kipaumbele. Amfikishe baba yake sehemu anayotaka midhali hakuna maasi hata kama atachelewa darsa.

Leo darsa zinarekodiwa na kuhifadhiwa. Mtu anaweza kusikiliza mkanda iwapo darsa itampita.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (04) http://alfawzan.af.org.sa/node/2047
  • Imechapishwa: 12/11/2016