69. Alichokifanya ili mke asifunue uso wake

2 – Qaadhwiy Abu ´Abdillaah Muhammad bin Ahmad bin Muusa amesema:

”Nilihudhuria kikao cha Qaadhiy Muusa bin Ishaaq huko Rayy mwaka wa 286 wakati ambapo msimamizi wa mwanamke alimtaka mume wake kutoa mahari ya sarafu ya dhahabu 500, jambo ambalo mume alikuwa analipinga. Qaadhiy akasema: ”Mashahidi wako wako wapi?” Akajibu: ”Nimewaleta.” Qaadhiy akamwita mmoja katika wale mashahidi amtazame mwanamke na baadaye amwashirie juu ya ushuhuda wake. Shahidi yule akasimama na Qaadhiy akamwambia mwanamke yule: ”Simama.” Mume akasema: ”Mnataka kufanya nini?” Wakili akasema: ”Watamtazama mke wako hali ya kuacha uso wazi ili waweze kumtambua.” Mume yule akasema: ”Mimi namshuhudisha Qaadhiy ya kwamba ni juu yangu kutoa hayo mahari anayoyadai. Msifunue uso wake.” Mwanamke yule akarejeshwa na akaelezwa aliyoyasema mume wake. Ndipo mwanamke yule akasema: ”Mimi namshuhudisha Qaadhiy ya kwamba nimempa zawadi mahari hayo na nimeacha madai yangu duniani na Aakhirah.” Ndipo Qaadhiy akasema: ”Haya yanatakiwa yaandikwe katika maadili mema.”[1]

Haya yanafahamisha kuwa yale yanayofanywa hii leo na wanawake wenye kujiheshimu na wenye kujichunga na machafu ni jambo limewekwa katika Shari´ah na lenye kusifiwa, ingawa si la lazima. Bali mwenye kufanya hivo amefanya jambo lenye ubora, lakini hapana neno pia kwa kutolifanya. Kutokana na yaliyokwishatangulia inabainika kuthibiti kwa sharti ya kwanza juu ya vazi la mwanamke pale anapotoka nyumbani, nalo ni kwamba anapaswa kujisitiri mwili wake mzima isipokuwa uso na mikono yake.

[1] Taariykh Baghdaad (13/53).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 09/10/2023