68. Hafswah bint Siyriyn alijifunika uso wake

Katika Hadiyth hii kuna dalili ya wazi juu ya kwamba wanawake kufunika nyuso zao ni jambo lililokuwa la kawaida katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanawake wabora walifuata mwenendo huo baada yao. Hapa nitakuletea mifano miwili juu ya hilo:

1 – ´Aaswim al-Ahwaal amesema:

”Tulipokuwa tunaingia kwa Hafswah bint Siyriyn alifunika uso wake kwa jilbaab ambapo tukamwambia: ”Allaah akurehemu! Kwani Allaah (Ta´ala) si amesema:

وَالْقَوَاعِدُ مِنَ النِّسَاءِ اللَّاتِي لَا يَرْجُونَ نِكَاحًا فَلَيْسَ عَلَيْهِنَّ جُنَاحٌ أَن يَضَعْنَ ثِيَابَهُنَّ غَيْرَ مُتَبَرِّجَاتٍ بِزِينَةٍ

“Na wale wanawake wazee waliokatika hedhi ambao hawataraji kuolewa, basi hapana neno juu yao kupunguza baadhi ya nguo zao bila ya kudhihirisha mapambo yao.”

Bi maana jilbaab.” Akasema: ”Aayah inasema nini baada ya hapo?” Tukasema:

وَأَن يَسْتَعْفِفْنَ خَيْرٌ لَّهُنَّ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

”Na kama watajihishimu ni bora kwao. Na Allaah ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”[1]

Akasema: ”Inathibitisha kujisitiri.”[2]

[1] 24:60

[2] Ameipokea al-Bayhaqiy (7/93) kupitia kwa Sa´daan bin Naswr: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim al-Ahwal. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri. Sa´daan jina lake ni Sa´iyd ambaye mara nyingi anatambulika kama Sa´daan, kama alivosema al-Khatwiyb katika “Taariykh Baghdaad”. ad-Daaraqutwniy na wengine wamemzingatia kama mwenye kuaminika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 09/10/2023