Ndugu! Kimbilia kufanya matendo mema kabla ya wakati haujakupita. Hivi sasa uko na uchangamfu, nguvu na uwezo. Lakini kunaweza kufika zama ambapo hutoweza kufanya mtendo mema. Hivyo basi fanya haraka na uizoweze nafsi yako. Ukiizoweza nafsi yako kwa matendo mema hatimaye utazowea na itakuwia sahali kuyatekeleza. Na ukiizoweza nafsi yako kuzembea na uvivu utashindwa kutekeleza matendo mema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/45)
  • Imechapishwa: 09/10/2023