Mtu anapokuwa mkubwa na uhai wake ukawa mrefu anarudishwa katika umri wa udhalilifu kabisa kama alivyosema Allaah (´Azza wa Jall)[1]. Utamuona mwanaume ambaye alikuwa ni miongoni mwa wanaume wenye akili nyingi kabisa anarudi nyuma na kuwa kama mtoto mdogo. Bali anakuwa mtwevu kuliko hata mtoto mdogo. Kwa sababu mtoto mdogo hapo kabla alikuwa hajapata akili na hajui kitu. Lakini huyu baada ya kuwa alikuwa ameshakuwa ni mtu mwenye akili na kuyaelewa mambo kisha anarudishwa katika umri wa udhalilifu kabisa, jambo ambalo linakiuwa ni baya zaidi kwake.

Ndio maana tunaona wale wanaorudishwa kwenye umri wa udhalilifu katika hali ya uzee wanakuwa ni wenye kuwaudhi wanafamilia wao zaidi kuliko maudhi ya mtoto mdogo. Kwa sababu wao hapo kabla walikuwa na akili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliomba kinga ya kurudishwa katika hali ya umri wenye udhalilifu[2]. Tunamuomba Allaah atukinge sote na kuturudisha katika hali ya umri wa udhalilifu. Kwa kuwa mtu akirudishwa katika umri wa udhalilifu anapata tabu sana na anawapatisha wengine tabu. Hali hufikia kiasi cha kwamba hata wale watu walio karibu zaidi na yeye wanatamani bora afe tu kutokana na jinsi amevyowaudhi na kuwapatia tabu.

[1]16:70

[2]al-Bukhaariy (2822) na Muslim (2706).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/42-43)
  • Imechapishwa: 16/10/2023