43. Ni ´ibaadah zipi zilizowekwa katika Shari´ah katika mwaka wa 2?

Swali 43: Ni ´ibaadah zipi zilizowekwa katika Shari´ah katika mwaka wa pili?

Jibu: Mwaka huohuo, tarehe 15 Sha´baan, kuliwekwa Shari´ah ya kuielekea Ka´bah, jambo lililopingwa na mayahudi.

Mwaka huohuo kuliwekwa Shari´ah ya kufunga Ramadhaan. Kabla ya hapo yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amefaradhisha ´Aashuuraa´.

Mwaka huohuo kulifaradhishwa Zakaat-ul-Fitwr, swalah ya ´Iyd na Zakaah ya mali ambayo mara nyingi imetajwa pamoja na swalah maeneo mengi ndani ya Qur-aan.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 108-109
  • Imechapishwa: 09/10/2023