68. Inapendeza kwa msafiri kufupisha swalah za Rak´ah nne

Swali 68: Tukiwa wasafiri na tukapita karibu na msikiti kwa mfano wakati wa swalah ya Dhuhr – je, imependekezwa kwetu kuswali Dhuhr pamoja na mkusanyiko kisha tuswali ´Aswr kwa kufupisha au tuiswali peke yetu? Je, tukiswali pamoja na mkusanyiko na tukataka kuswali ´Aswr tusimame papo hapo baada ya salamu kwa ajili ya kuharakisha swalah au tumtaje Allaah, tumsabihi na tuseme “Laa ilaaha illa Allaah” kisha tuswali ´Aswr?

Jibu: Bora kwenu ni kuswali peke yenu kwa kufupisha. Kwa sababu inapendekeza kwa msafiri kufupisha swalah za Rak´ah nnenne. Mkiswali pamoja na wakazi basi itakulazimu kuswali kwa kukamilisha. Hivo ndivo zilivyosihi Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mkitaka kukusanya basi imesuniwa kwenu kuharakisha jambo hilo kwa ajili ya kutendea kazi Sunnah, kama ilivyokwishatangulia katika jibu la swali lililotangulia baada ya kusema:

أستغفر الله. أستغفر الله. أستغفر الله. اللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

 “Namwomba Allaah msamaha. Namwomba Allaah msamaha. Namwomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Lakini msafiri akiwa peke yake basi analazimika kuswali pamoja na mkusanyiko ya wakazi na aswali kwa kukamilisha. Kwa sababu kuswali kwa kukamilisha ni miongoni mwa mambo ya wajibu na kufupisha swalah ni jambo linalopendeza tu. Kwa hivyo ni lazima kutanguliza jambo la wajibu juu ya jambo lililopendekezwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 71
  • Imechapishwa: 13/09/2022